KISA NA MKASA

           HAYA MAJINA TUNAYOPEWA TUYACHUNGUZE


Jamaa mmoja  wilayani  bagamoyo alikamatwa pamoja na wenzake kwa mama muuza gongo wakinyonya tartiiibu kitu hiyo haramu bila  wasi wasi wowote.
Baada ya kufika polisi mambo yalikuwa hivi…………
Afande:Mzee unaitwa nani?
Jamaa:Matatizo.
Afande:Nani?
Jamaa:Matatizo afande.
Afande:Matatizo?!,Matatizo nani?!..
Jamaa:Matatizo kesi!
Afande:Kama unajua kesi ni matatizo mbona unakunywa gongo hadharani?
Jamaa:kesi baba yangu matatizo babu yangu,nimepewa jina la babu naitwa Matatizo Kesi  Matatizo!
Afande:Ok! Unafanya kazi gani?
Jamaa:Baba wa nyumbani.
Afande:eeh! Ebo!
Jamaa:Mke wangu ndio anafanya kazi,anauza embe.
Afande:Mzee umri wako…?
Jamaa:Hapo afande kwa kweli nimesahau naomba uniachie kidogo nika muulize mama mzazi,pombe yangu si mmeikamata?Nitarudi tu....
                     

HII IMETOKEA KWA MARA YA KWANZA

Hivi karibuni kumekuwa na njaa katika sehemu sehemu nchini,Basi hii imetokea kwa mara ya kwanza kwa mganga wa kienyeji  katika moja ya maeneo yaliokumbwa na  njaa kali!.
Mganga:Tatizo lenu dogo nimeliona,ndio dogo saana,mbhluuu,mbluuh….
Mteja:ndio mganga hatulali…tusaidie baba……
Mganga;Basii usiseme maneno mengi mizimu imeisha ona…sasa kaleteni jogoo             mweusi..mbhluuuuuu….mbhluuuu….
Mteja:Mganga kweli kama tatitzo letu umeliona haujaona…na maanisha mizimu haijaona kama hamna kuku hapa kijijini?kuku tutapata wapi na njaa hii.. hauoni..(kabla hajamalizia)
Mganga;Ndio,mbluuu,mbluu….mizimu imeona njaa kali…ime…ime….imeagiza mlete matembele
Mteja:Mganga matembele yenyewe tutayatolea wapi pote pamekauka
Mteja mwingine:Hata yale ya chooni yamekauka hali mbaya!....
Mganga:kweli hali mbaya mizimu imegoma njoeni kesho.

Hii haijawahi kutokea kweli njaa noma!mganga kuagiza matembele!



JAMAA AMDAI NESI URODA

 Baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria, jamaa  aliye fahamika kwa jina moja la Mandondo,alienda hospitali Fulani kubwa hapa jijini Mwanza(jina tumelihifadhi) Kutokana na elimu kubwa ya customer care jamaa alipokelewa mapokezi kwa lugha ya upole na ustaarabu ambayo hakuwahi kuisikia hata kwa mke wake.
Baada  ya kumuona daktari alienda maabara akakutwa  ana malaria mambo yakawa hivi,
Daktari: Ndugu,mkojo wako msafi ila una malaria,utaenda  chumba hicho hapo kushoto nesi atakupa dawa hizi nilizo kuandikia na ORDAR.
Jamaa:Na nini dokta?!.......
Daktari;Na  Ordar…au hautumii?
Jamaa:Natumia…..Natumia Dokta..
Jamaa alienda kwa nesi huku akitabasamu na kuwaza..kumbe ndio mtindo wao ndio maana wanatabasamu sana.
Jamaa;Dokta kasema unipe dawa  hizi ..naaa…naaa..na.Uroda.
Nesi:Na nini?
Jamaa;hata mi nilishangaa, kaniambia unipe dawa hizo na uroda!
Nesi:Hapana kaka sio Uroda ni Ordar dawa ya malaria,si una malaria wewe?nesi aliuliza huku akitabasamu
Jamaa;Ndio,sa…sa.samahani mama.









No comments:

Post a Comment